Internet ni kitu cha muhimu sana na ambacho karibu watumiaji wote wa smartphones hukizingatia kwanza. Lakini kuna baadhi ya watumiaji wa smartphones wamekuwa wakikubwa na matatizo ya simu zao kutomuwa na mtandao wa internet ambao haueleweki mara 2g mara 3g, 4g pasipo ruhusa ya mtumiaji.
UNAJUA KWA NINI HALI HII HUTOKEA???!!. Frequencies za mtandao hubadilishana kutokana na matumizi ya internet kwenye eneo husika, hivyo suala la smartphone kujichagulia mtandao yenyewe hutegemeana frequencies za mtandao upi unaokuwa na nguvu ndani ya muda husika.
Kama frequencies za 2g, 3g au 4g Zitakuwa na nguvu basi smartphone yako itakachagua mtandao wa kutumia yenyewe.
KAMA SMARTPHONE YAKO INAJICHAGULIA 2G, 3G, AU 4G BILA WEWE KUPENDA BASI FANYA YAFUATAYO
Kama unatumia smartphone ya >>>>>>>>>
#ANDROID
FANYA HIVI KIURAHISI:
- NENDA SEHEMU YA KUANDIKIA NAMBA
- BONYEZA >>> *#*#4636#*#* kama inakataa download application ya Phone testing
- Yatatokea machaguo kadhaa chagua #Phone information
- Shuka chini kabisa mpaka mpaka sehemu iliyoandikwa Set preferred network type gusa chini yake utaona machaguo ya mtandao yenye kumanisha aina ya mtandao wa internet. chagua >>>>>>>>
- GSM only kwa 2G peke yake
- WCDMA only kwa 3G peke yake
- LTE only kwa 4G peke yake
## ZINGATIA:
Njia hii inafanya kazi kwenye simu nyingi za android lakini baadhi ya smartphones kama Samsung inakataa. Hivyo kama una simu ya jinsi hii na unatumia Android fanya rahisi ifuatavyo >>>>>>>>
- Nenda kwenye Settings za simu
- Angalia kipengele cha Network
- Chagua Mobile network
- Bofya Network mode
- Yatatokea machaguo ya mitandao ya internet kulingana na uwezo wa simu yako yaani >>> 2G, 3G, na 4G
Comments
Post a Comment