Skip to main content

KILA SIKU FIKIRIA NA JIFUNZE KWA BIDII UTAFANIKIWA





          JIFUNZE KWA WALIOFANIKIWA
Ukitaka kufanikiwa kaa karibu na jifunze kwa waliofanikiwa, hili ni
jambo wengi wanalisahau sana wanapo kuwa wanatafuta mafanikio.
Mafanikio hayaji tu kutokea hewani kimiujiza, kiuhalisia wote tunajua
ukitaka kufanikiwa lazima ufanye baadhi ya mambo yafuatayo;
– uwe na wazo la biashara au mradi
– mtaji
– ujitume kwa bidii
– uwe mvumilivu sio mwepesi kukata tamaa
– kujiamini
– na mengineyo unaweza kuongeza kwenye boksi la maoni
Lakini pamoja na kufanya hayo yote bado unahitaji kuwa na MENTOR,
yani mtu au watu wanaofanya mradi kama wako lakini wao tayari
wamekwisha fanikiwa na wana uzoefu wa hilo jambo, itakuwa rahisi
kwako kupata ujuzi na uzoefu kutoka kwao. Unaweza ukajikuta
makosa walio fanya wao wewe ukayaepuka maana una mtu wa
kukupa mwongozo
Kumbuka pia watu walio karibu na wewe wana nafasi kubwa ya
kukujenga au kukubomoa, maana ukikaaa karibu na wajasiriamali
waliofanikiwa ni rahisi kwao kukupa moyo unapokabiliana na
changamoto za kijasiriamali . Ila ukizungukwa na watu wenye
mtazamo tofauti na wala hawajui ujasiriamali ni nini, kukatishwa
tamaa ni rahisi sana ukishindwa kidogo watakwambia bora uache tu,
tafuta kitu kingine cha kufanya.
KATIKA MAISHA UNAWEZA KAHAMA KUTOKA ULIKOKUWA NA
KWENDA KATIKA MAISHA MAPYA NA KUPATA MAFANIKIO.
TUJIFUNZE
KUHUSU KILIMO
MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KABLA HUJAINGIA KATIKA
KILIMO CHA BIASHARA.
Kabla haujaamua kuingia katika kilimo cha biashara inakupasa
kwanza ufahamu mambo muhimu ambayo yatakusaidia katika
shughuri yako ya kilimo husika.
Kwani yakupasa kutambua kila kazi ya kuingiza kipato ina
changamoto zake na kilimo ni moja ya kazi yenye changamoto nyingi
ambazo yakupasa nyigine ujipange jinsi ya kukabiliana nazo kabla ya
kuaingia katika kilimo husika.
Mambo hayo muhimu ni
1>UTAYARI KUINGIA KATIKA KILIMO
Inakupasa kabla hujajiingiza katika kilimo uwe tayari wewe
mwenyewe kuamua kuanza kufanya kufanya kilimo husika,Kwa
maana nyingine namaanisha maamuzi yako ya kuingia katika kilimo
yatokane na uchaguzi wako mwenyewe baada ya kuangaliaya na
kuona kilimo ni moja ya jambo litakaroboresha kipato chako.Ili
kuepuka kujiuliza uliza maswali ya uamuzi wako wa kwanini na nani
amekushauri kuingia kufanya shughuri hiyo ya kilimo husika,Hivyo
utayari wako utakusaidia kuongeza ari na juhudi zaidi katika kazi
yako na kukupunguzia kukata tamaa njiani.
>UCHAGUZI WA KILIMO KINACHOKUFAA
Kabla ya kuingia katika kilimo lazima kwanza ufanye uchaguzi wa
kilimo gani ambacho utafanya.Katika Uchaguzi lazima uchague kitu
ambacho utakuwa tayari kukifanya bila kupata pingamizi la utayari
wa kufanya kilimo hicho.Katika uchaguzi unaweza kuchagua kilimo
mchanganisho kwa maana kulima mazao na kufuga mifugo au kulima
mazao/kufuga mifugo tuu.
Na hapa katika uchaguzi ukichagua kilimo ambacho si sahihi kwako
ndipo ambapo husababisha changamoto nyingi katika kilimo chako
hapo baadaye.Hivyo uwe makini katika kuchagua Mazao/Zao,Mifugo/
Mfugo sahihi kwako kutokana na utakavyojiangalia utayari wako.
3>UTAFITI NA USHAURI WA GHARAMA JUU YA KILIMO
ULICHOKICHAGUA
Baada ya kufanya uchaguzi wako inakupasa ufanye utafiti wa
gharama utakazoweza kuzimudu katika kilimo chako.Hili litaendana
na Ushauri wa Jinsi gani ya kuweza kufanya kilimo chako kwa
gharama nafuu zaidi ili kama ikitokea hasara uwe na uwezo wa
kuikabili vizuri.
4>PANGA BAJETI YAKO KABLA HUJAANZA KILIMO
Yakupasa upange bajeti yako kabla hujaanza kilimo kwa kuangalia
utafiti na ushauri wa gharama juu ya Kilimo ulichokichagua.Hi
itakusaidia katika manunuzi na malipo ya huduma muhimu katika
shughuri zako kwani utakuwa umejipanga mapema kukabiliana na
matatizo yatakayohitaji fedha ya mfukoni kwa ajili ya huduma kama
madawa,mbegu n.k
Kumbuka* malipo ya watakaohudumia kilimo chako usiyasahau
katika bajeti yako na yataendana kulingana na idadi ya utakaowaajiri.
5>USIMAMIZI MZURI
Baada ya Kupanaga mipango yako usisaha katika kupanga vizuri
usimamizi wa kilimo chako na hapa ukifanya makosa kamwe
hutoweza kufanikiwa na kuishia kukiona kilimo hakifai hata kama
ulitoa gharama zote zilizohitajika wenyewe wanasema uchungu wa
mwana ajuaye mzazi,,wakulima tunasema uchungu wa kilimo aujuaye
mkulima,Msemo huu,hii ianamaanisha uangalizi wako kwa ukaribu
katika kilimo chako unahitajika zaidi kuliko kuwa mtu wa kuagiza tuu
bila kufuatilia maendeleo ya kilimo chako wakati kinafanyika.
6> TAFUTA USHAURI WA UTAALAM WA KILIMO ULICHOKICHAGUA
Kabla hujaanza usisite kutafuta ushauri wa kitaalam wa kilimo
ulichokichagua.Ili uwe karibu na kugundua tatizo katika kilimo chako
kabla hujachelewa sana kupata athari ya tatizo husika.Na pia hili
litakusaidia kufanya kilimo chako kwa uhakika zaidi.
7> ANZA KILIMO CHAKO KWA UHAKIKA
Mwisho baada ya kupitia hatua hizo juu anza kufanya kilimo chako
kwa uhakika zaidi na Pia huku unatambua kilimo nacho ni biashara
kama zilivyo biashara nyingine hivyo uwe makini katika kilimo chako
ili kujiepusha na changamoto zitakazojitokeza katika kilimo chako na
changamoto hizo zisiwe kikwazo katika kukuzuia kuendendelea na
kilimo chako.
NAKUTAKIA KILIMO.CHEMA

Comments

Popular posts from this blog

TENGENEZA KIPATO KUPITIA FACEBOOK

Mara nyingi wengi wetu tumezoea kutumia social network mbalimbali kama kujiburudisha bila kujua kwamba kila mtandao wa kijamii una njia ya kukutengenezea kipato kikubwa. leo nimeona nianze kukufundisha njia ya kuingiza pesa kupitia facebook  ILI KUTENGENEZA KIPATO KWA NJIA FACEBOOK UNATAKIWA KUWA NA VITU VIFUANTAVYO 1. Unatakiwa uwe na accont ya bank 2.Uwe na creditcard ya mastercard au visacard  3. unatakiwa  uwe na account ya paypal kwa ajili ya kupokea payment kutoka kwenye mtandao wowote wa kijamii utakaojiunga nao ukiwa na hivyo vitu unaweza kutengeneza pesa nyingi kwa mwezi mmoja CHANZO CHA KIPATO Vipo vyanzo vingi au njia nyingi za kutengeneza kipato ndani ya fb leo nitaelezea njia ambayo ni rahisi sana ambayo mtu yeyote anaweza kuitumia bila kuwa mtaalamu sana  njia hiyo ni ya kulipwa kwa like  kwa hiyo unalipwa kwa kupata like unazozipata kwenye page yako au group ndani ya facebook zipo njia kuu mbili za kufanya trick upate like n...

JINSI YA KURUDISHA DOCOMENT ZILIZOFUTIKA KATIKA SIMU

Sio kitu kipya wote tumeshawahi fanya, kwa bahati mbaya tulishawahi kufuta taarifa zetu kama vile picha au hata video. Kama ikitokea hivyo tena usikasirike, ITphidel nakuletea njia. Sawa kama nlivyosema kuwa unaweza ukapata taarifa zako zote ambazo ulifuta kwa bahati mbaya lakini kabla ya kuzipata kuna mambo inabidi uyafanye • Usihifadhi (save) kitu kingine chochote katika simu kifaa chako au izime mpaka ukiwa unampango wa kufufua vitu vyako • Zima WiFi na njia za mawasiliano za 2G/3G ili masashisho (update) yanayofanyikaga automatiki yasifanyike. Kumbuka kama yakifanyika, mafaili mapya yanaweza jiweka juu ya yale ambayo unataka kutafufua Tuifahamu Njia Kama Mafaili Yako Yapo Katika Memori Kadi Ukishaona mafaili yako yamefutika bahati mbaya – au hata kwa makusudi – kitu kinachofuata ni kuunganisha kompyuta yako na simu kwa kutumia USB. Kuna baadhi ya matoleo ya vifaa vya android, ukichomeka USB katika kompyuta haijionyesha katika mfumo ule wa ‘kuonekana kama umechomeka Flash tu...

App 5 Muhimu Za Kuwa Nazo Katika Simu Janja yako!

Kwa watu wengi sana simu janja zao ndio kila kitu (ukitaka kuamini angalia sura zao pindi wanapoibiwa) unaweza kutumia simu hizo kufanya karibia kila kitu Kuanzia kwenye kufanya manunuzi ya vitu,kuelekezwa mitaa, kuangalia barua pepe na hata kuwasiliana na ndugu pamoja na jamaa. Mambo ya kufanya na simu janja ni mengi sana hata nikitaja sitayamaliza. Ukiachana na kila kitu ambacho simu janja yako au tablet inachoweza kufanya inabidi uhakikishe kuna App za muhimu katika simu yako ambazo zitarahisisha ufanyikaji wa mambo hayo kwa namna ya kipekee. KUTAFUTA SIMU ILIYO POTEA/IBWA Hivi unajua hakuna mda mzuri wa kuibiwa? Chochote kama kweli ni chako kikiibiwa lazima uumie sana. Nshashuhudia dada kaibiwa simu akaanza kulia! (hizi smatifoni bwana, Hah!). hapo awali ilikua kama mtu ukiibiwa au ukipoteza simu yako matumaini ya kuipata tena hakuna kabisa Lakini asante kwa Find My iPhone (ya iOS) na Android Device Manager (ya android) sasa tuna matumaini ya kupata vitu...