Watu wengi wanashindwa kujua maana halisi ya mtaji.
Wengi wanafikiri labda mtaji lazima iwe fedha, lakini kiukweli mtaji ni
zaidi ya fedha. mtaji inaweza kuwa ni vingi vingi mbali na fedha.
Mtaji ni nini?
Mtaji ni kitu chochote ambacho unaweza kutumia kuanzishia biashara
yako na kupata faida. kwa hiyo mara nyingine sio fedha inaweza kuwa ni
kitu fulani cha aina fulani, linaweza kuwa ni jambo fulani, mahusiano ,ni
watu, ni mtandao ulionao, labda ni wazo zuri sana unakuwa nalo, ama ni
jina jema katika jamii.
Kwa hiyo vyote hivi vinaweza kuwa ni mtaji wa kuanza na kudumu
ambavyo vinaweza kubadilishwa na kuwa katika form ya pesa.
Kumbe mtaji sio fedha tu.
Njia hizo ni kama ifuatavyo
1. Mtaji mbadala
Tunapozungumzia mtaji mbadala hapa tunamaanisha ni yale mambo
ambayo ingebidi utumie fedha hutatumia fedha , utatumia kwa mfano
nguvu zako mwenyewe, au jasho mwenyewe,, au maarifa fulani,au jina
mtu mwingine, au utakopa ,au kuazima , au ubunifu, ndio unakuwa tayari
umetumia mtaji mbadala. kwa mfano kipaji ulichonacho au uzoefu fulani
au uwezo binafsi uliojijengea n.k
A. Kipaji Ulichonacho:
Mfano Masanja leo hii ni maarufu sana kwa sababu ametumia kipaji
chake cha kuchekesha kuwa mjasiriamali mzuri, Hakuhitaji pesa kufanya
ujasiriamal wake.
B. Uzoefu ulionao
Hili watu hawajui kama ni mtaji mbadala utakuta wanasema '' AAah
mimi ni mwalimu tu wa chekechea'' nifanye biashara gani, akasema sina
mtaji'' nikamwambia " huna sebule? akasema 'ninayo ' nikamwambia
anzia hapo hapo, na kufikia leo hii dada Hadija ana shule 3 za
chekechea Dar es salaam
C. Maarifa uliyonayo ambayo wengine hawana
Tunaposema maarifa mbalimbali mfano leo hii watu wananilipa kwa
kusikiliza kwa sababu nina maarifa ya kutatua matatizo ya watu
waliyonayo kijasiriamali.
D. Elimu yako
Mfano una cherehani iko ndani, kwa nini usianze kushona? wamiliki
wengi wa makampuni makubwa ya ushonaji walianza hivyo hivyo
2. Kupata mtaji kwa ndugu, jamaa na marafiki
Watu wengi wanakuwa kwenye umaskini wakati wamezungukwa na
ndugu matajiri kisa wanaona aibu kuomba msaada, lakini amini usiamini
watu wengi wametajirika kupitia ndugu, jamaa na marafiki,
Mfano mtu tajiri kuliko wote barani Afrika kutoka Nigeria ndugu Dangote
yeye alivyotaka kuanza ujasiriamali aliomba msaada toka kwa mjomba
wake ambaye alimuazima kama milioni 3 hivi kwa kuwa aliona fursa
kwenye mambo ya ujenzi (cement).
Dangote akaanza kununua cement na kuuza leo hii ndugu Dangote
amekuwa bilionea ambaye amewekeza sana barani Afrika anauza
cement, unga , mchele, mafuta, sukari na saa hivi anauza mafuta kule
Africa Magharibi hata hapa Tanzania tuna kiwanda chake kule Mtwara,
Kuomba msaada sio ishara ua udhaifu bali ni ishara ya nguvu kwamba
unajiamini ndio maana unaomba msaada. kumbuka kwenye neno
UJASIRIAMALI kuna neno Jasiri pia, huwezi kuwa na mali bila kuwa
jasiri.Umezungukwa na watu waliobarikiwa usisite kuwaambia
wakusaidie ,.
3. Kujiwekea akiba
Watu wengi sana hapa kwetu Tanzania ukiwaambia weka akiba
wanakwambia mimi siwezi kuweka akiba, sina utamaduni wa kuweka
akiba,
Hivyo mi nakushauri anza leo kujifunza kuweka akiba, ni ngumu sana
kufika juu bila kuweka akiba kwa mfano kama umeajiriwa na unajua
biashara fulani inataka milioni 2 ili kuifanya na wewe mshahara wako ni
laki 4,
Kwa nini basi kila mwezi usiweke laki 1 pembeni, ndani ya miaka miwili
utakuwa na milioni 2.4 huo ni mtaji wako wewe mwenyewe.
Usisite kuanza kidogo kwa kuweka akiba polepole mpaka ufike huko
unakoenda
4. Pata Mtaji kwa njia ya kudunduliza
Hii njia ya kudunduliza ndio njia ambayo ni nyepesi kabisa ambayo watu
wengi hawaioni, ukiamua kutumia njia hii kamwe huwezi kukosa mtaji,
Hii ina maana unaanza katika hali ya chini kabisa ya kufanya kitu
chochote halafu ile faida unayoipata hauitumii bali unaiwekeza kwenye
biashara yako.Tuone mfano wa dada Christine ambaye ni mfano mzuri
wa mtaji wa kudunduliza
Christine Momburi alikuwa amejifungua na mume wake walikuwa
amemuachisha kazi kwa hivyo maisha hayakuwa mazuri sana,
Sasa siku moja walitembelewa na mgeni nyumbani kwao yule mgeni
alipotaka kuondoka alimpa Christina shilingi 700 ili anunue maziwa ya
mtoto, baada ya yule mgeni kuondoka Christina alijiuliza "Je aitumie ile
sh 700 kununua maziwa au afanyie nini hasa ili iweze kubadili maisha
yake?"
Christina alijiuliza sana baadae akaamua kuichukua ile hela aende
sehemu akanunue nyanya chungu na mboga mboga kwa bei ya jumla.
Akazinunua akaenda kuuza, kwa siku ya kwanza ikatoka sh 700 kwenda
1500 akaongeza mtaji wake, ilikufupisha stori baada ya wiki moja
Christina akawa na mtaji wa sh 25000/=.
Siku moja akasikia kuna mahali wanajenga wanataka mama lishe wa
kuwapelekea chakula akachukua ile tenda akawa anawapelekea chakula,
baadae akasikia kuna sehemu wanataka mtu wa kuwapelekea sare za
shule. akawa anazidi kukua na kukua na hivi sasa Christina amekuwa ni
mjasiriamali mkubwa pale Moshi ana maduka makubwa sana na
amehojiwa na vyombo vya habari mbalimbali na yeye amekiri kwamba
kudunduliza ndio kuliko mtoa.
Sasa swali la msingi nalotaka nikuulize ni swal lifuatalo
Swali, Ni je ni Sh 700 ngapi zimepita mikononi mwako? Je ni Sh 7000
ngapi zimepita mikononi mwako? Je ni Sh 70000 zimepita mikononi
mwako? vipi kuhusu laki 7 au milioni 7 ngap zimepita mikononi mwako?
Mara nyingi tumeidharau fedha na kuona ni ndogo lakini kumbuka
nilishasema siku za nyuma kuwa kila shilingi inayopita mikononi mwako
ni itazame kwa jicho la kimilionea.
Nikukumbushe kuwa tajiri kuna maumivu ambayo utayapitia, watu wengi
hawataki kupitia maumivu ndio maana watu wachache sana wanakuwa
matajiri., watu wengi wanapenda utukufu lakini hawataki kubeba
msalaba.
Hivyo usidharau pesa bali fikiria kwa ubunifu jinsi ya kuizalisha fedha
hiyo.
5. Pata Mtaji mdogo kupitia wawekezaji
Wakati mwingine kutokana na mazingira uliyonayo unaweza ukagundua
kwamba una wazo zuri sana la biashara lakini hauna mtaji, hapa jambo
la msingi ni kuangalia unaweza kumpata vipi muwekezaji ambaye
atataka faida, ni afadhali ukawa na wazo ukawashirikisha wengine
wakakupa mtaji halafu mkagawana faida kuliko kufa na wazo lako zuri,.
sisi watanzania tupo nyuma sana katika suala la kufanya biashara
pamoja ( Partinership) tofauti na wakenya.
Mfano mzuri Elisha yuko Iringa, yeye aliwaza kuanzisha kiwanda cha
mbao hizi nguzo za umeme, bahati mbaya hakuwa na mtaji wa kutosha
akaamua kuongea na marafiki zake zaidi ya 10 akamshawishi kila rafiki
yake awekeze kiasi kadhaa cha fedha na kumpatia hisa kwenye kile
kiwanda chake, rafiki zake walikusanyika wakatoa fedha na sasa
kiwanda kimeanzishwa na kinakaribia kutoa nguzo wakati wowote
kuanzia sasa.
Je wewe una weza ukatumia njia hii? Je una wazo ambalo unajua kabisa
hili wazo nikipata wawekezaji wa nanmna hii? masharti yake yanaweza
kuwa magumu sababu unaweza kuambiwa uandike mchanganuo wa
biashara unao eleweka, na wazo lako la biashara lionekane limetulia
kabisa.
Lakini ni afadhali ukapitia mchakato huu kuliko kuwa na wazo zuri
halafu wewe huna fedha. na kumbe ungeweza kutoa ajira na kulipa kodi
kwa nchi hii na kufanya wenzako wakanufaika na wazo ulilonalo.
6.Kupitia Taasisi za kifedha
Mada hii ni ndefu sana
Lakini nataka tu ujue ili benki ikukope inahitaji uwe na biashara ambayo
imeshakuwepo kwa takribani miezi 6 au zaidi, pia watahitaji uwe na
mzunguko mzuri wa fedha unaoeleweka, uwe na dhamana ambayo
unaiweka ili kama unashindwa kulipa waweze kuichukua ile dhamana,
watahitaji uwe umefanya usajili rasmi wa biashara yako., uwe na
account ya benk n.k
Sasa basi kwa kuwa watu wanaogopa kwenda benki kutokana na yote
haya ndipo unaweza kujaribu kutumia microfinances, hizi ni taasis za
kifedha ambazo hutoa mikopo midogo midogo, kwa hiyo angalia kama
huko ndiko unapoweza ukaponea.
7. Mtaji kwa njia ya Mgavi ( Supplier Financing)
Hii ni njia ya uhakika ya kupata mtaji wako. Naomba nitoe stori halisi ,
Miaka mingi iliyopita kijana mmoja anayeitwa Reginald alikuwa
anatafuta kalamu za kuandikia mtaani kwake, lakin bahati mbaya baada
ya kutafuta sana kwa muda mrefu alikosa kalamu pale mtaani kwake,
Jambo hilo lilimfanya aweze kushangaa sana na kujiuliza hivi kweli
inawezekana vipi hakuna kalamu hapa mtaani? kwa hyo hilo likamfanya
aanze kutafuta mbinu na maarifa ya yeye kuwa mtu ambaye analeta
kalamu Tanzania.
Baada kufanya uchunguzi kwa marafiki mbalimbali wakati huo yeye
alikuwa muhasibu tu, akaambiwa Mombasa kuna mtu ana kiwanda cha
kalamu na baada ya kufanya mazungumzo na yule ndugu ikaonekana
bwana Reginald angeweza kuwa anaingiza kalamu hapa Tanzania lakini
hakuwa na mtaji, ndipo hapo ilibidi atumie mali kauli yaani awashawishi
wale watu wampatie zile kalamu azilete hapa, aziuze halafu aweze
kurejesha fedha na kuchukua faida yake.
Hivyo akaanza hiyo biashara kwenye chumba chake kidogo sebuleni
akisaidiwa na familia yake baadae wahamia nje wakatengeneza banda la
mabati tayari ikawa ndio kiwanda kwa ajili ya kupaki zile kalamu kwa
pamoja.
Mwaka huo huo wa kwanza bwana Reginald alipata faida kubwa sana
takriban mabilion ya shilingi.

Comments
Post a Comment