Skip to main content

MAARIFA:ITAMBUE MITI MAARUFU HAPA TANZANIA


u
Ifuatayo ni baadhi ya miti maarufu Tanzania iwe ili pandwa au ilijiotea
yenyewe.Baadhi ya miti imekuwa kivutio kutokana na historia na faida
yake kwa jamii.Miti ni viumbe hai vinavyojumuisha uzito hai kama ilivyo
kwa wanyama na uhai wake ni muhimu kwa dunia endelevu.Miti
imechangia katika dhima mbalimbali iwe historia
,elimu,utamaduni,harakati na utalii.Miti ifuatayo ni maarufu kutokana na
kuvutia watalii,wasomi na watu wadini na wa matambiko kutoka maeneo
tofauti Tanzania na dunia kwa ujumla.
Mdegree Tree (FICUS)
Mti huu unapatikana katika chuo kikuu cha Dar es Salaam ni mti
maarufu uliopandwa mwaka 1960 na raisi wa kwanza wa Tanzania Mwl
J. # Nyerere .Mti huu ulioko mbele ya ukumbi wa Nkuruma hall unaopatia
wanafunzi kivuli cha kusoma na kupata degree zao.Mahali pa mti huu
ndipo harakati za maandamano na migomo ya wanafunzi
huanzia.Mahali hapa pa mti huu pana mazingira mazuri ya kusomea
pamoja na mtandao wa bure.
Image
Mwembe waliokutana Dr David Livingstone na Stanley
Mwembe huu ulioko # Ujiji # Kigoma karibu na jumba la makumbusho
la # Dr Livingstone ndipo walipokutana wachunguzi karne ya 19.Mwembe
huu uko chini ya idara ya Mali kale kama kumbukumbu ya historia ya
bara.Mwembe huu mpaka leo umesimama na kuvutia watu mbalimbali
duniani.
Mbuyu wa kujificha Majangili (poachers hide)
Mti huu aina ya mbuyu(Adansonia digitata) unapatikana katika hifadhi
ya taifa Tarangire.Hapo zamani mbuyu huu ulikuwa unatumika pango la
kujificha majangili waliokuwa wanawinda wanyamapori ndani ya
hifadhi.Mbuyu huu katikati unapango ambalo wanaweza kuingia takribani
watu arobaini.Mbuyu huu unavutia watalii wanaotembelea hifadhi
ya # Tarangire na ni mojawapo ya rasilimali ya utalii inayopatikana
katika hifadhi ya Tarangire.
Mbuyu wa kanisa
Mti huu ni maarufu na muhimu kwa kanisa katoliki na historia yake ya
kuenea kwa ukiristo Afrika Mashariki.Mbuyu huu unaopatikana katika mji
mkongwe wa # Bagamoyo ulipandwa mwaka 1860 na padri Anthony
Horner kwa misheni ya Katoliki Bagamoyo.Mti huu jinsi unavyokuwa kwa
Wakatoliki ndo jinsi imani ya Kanisa Katoliki linavyoenea Afrika
Mashariki.Mti huu una baki ya mjororo uliokuwa unatumika kufunga
punda wa muuguzi Madame de Chevalier mnamo mwaka 1895.
Mvule wa Ajabu
Mvule wa Ajabu ni mti maarufu unaopatikana katika hifadhi ya msitu wa
Rau # Moshi inasemekana na Tanzania Tourist Board kwamba ndo mvule
wenye umri mrefu # Afrika .Mti huu wenye umri takribani miaka 194
umeweza kudumu umri huu katikati ya miti mingi muhimu ya mbao na
sgughuli za binadamu kutokana na mila na desturi za wananchi
wanaozunguka msitu huu.Historia inayo kwamba mti huu ulikuwa
ukikatwa unatoa damu pamoja na shughuli za matambiko mti huu
ukapona na kutimiza umri mrefu kati ya miti ya mivule Tanzania.Hii
inaonyesha kwamba mila na desturi zetu za Mwafrika zilikuwa
zinasaidia kuhifadhi mimea na wanyama toka kale.Mti huu ni rasilimali
ya utalii katika # Msitu wa Hifadhi Rau.ndio maana Rau Rau eco and
cultural tourism programme wanaendeleza mpango wao mahsusi wa
utalii ikiwa kivutio kikubwa ni Mvule wa Ajabu.
Image
Hii ni baadhi ya miti maarufu michache inayopatikana # Tanzania na ipo
katika uhifadhi uwe wa Mali Asili au Mali Kale.Makala ni maalumu kwa
kutambua michango miti katika historia,tamaduni na maisha yetu ya kila
siku.Mimi ni Mkumbatia Mti

Comments

Popular posts from this blog

TENGENEZA KIPATO KUPITIA FACEBOOK

Mara nyingi wengi wetu tumezoea kutumia social network mbalimbali kama kujiburudisha bila kujua kwamba kila mtandao wa kijamii una njia ya kukutengenezea kipato kikubwa. leo nimeona nianze kukufundisha njia ya kuingiza pesa kupitia facebook  ILI KUTENGENEZA KIPATO KWA NJIA FACEBOOK UNATAKIWA KUWA NA VITU VIFUANTAVYO 1. Unatakiwa uwe na accont ya bank 2.Uwe na creditcard ya mastercard au visacard  3. unatakiwa  uwe na account ya paypal kwa ajili ya kupokea payment kutoka kwenye mtandao wowote wa kijamii utakaojiunga nao ukiwa na hivyo vitu unaweza kutengeneza pesa nyingi kwa mwezi mmoja CHANZO CHA KIPATO Vipo vyanzo vingi au njia nyingi za kutengeneza kipato ndani ya fb leo nitaelezea njia ambayo ni rahisi sana ambayo mtu yeyote anaweza kuitumia bila kuwa mtaalamu sana  njia hiyo ni ya kulipwa kwa like  kwa hiyo unalipwa kwa kupata like unazozipata kwenye page yako au group ndani ya facebook zipo njia kuu mbili za kufanya trick upate like n...

JINSI YA KURUDISHA DOCOMENT ZILIZOFUTIKA KATIKA SIMU

Sio kitu kipya wote tumeshawahi fanya, kwa bahati mbaya tulishawahi kufuta taarifa zetu kama vile picha au hata video. Kama ikitokea hivyo tena usikasirike, ITphidel nakuletea njia. Sawa kama nlivyosema kuwa unaweza ukapata taarifa zako zote ambazo ulifuta kwa bahati mbaya lakini kabla ya kuzipata kuna mambo inabidi uyafanye • Usihifadhi (save) kitu kingine chochote katika simu kifaa chako au izime mpaka ukiwa unampango wa kufufua vitu vyako • Zima WiFi na njia za mawasiliano za 2G/3G ili masashisho (update) yanayofanyikaga automatiki yasifanyike. Kumbuka kama yakifanyika, mafaili mapya yanaweza jiweka juu ya yale ambayo unataka kutafufua Tuifahamu Njia Kama Mafaili Yako Yapo Katika Memori Kadi Ukishaona mafaili yako yamefutika bahati mbaya – au hata kwa makusudi – kitu kinachofuata ni kuunganisha kompyuta yako na simu kwa kutumia USB. Kuna baadhi ya matoleo ya vifaa vya android, ukichomeka USB katika kompyuta haijionyesha katika mfumo ule wa ‘kuonekana kama umechomeka Flash tu...

App 5 Muhimu Za Kuwa Nazo Katika Simu Janja yako!

Kwa watu wengi sana simu janja zao ndio kila kitu (ukitaka kuamini angalia sura zao pindi wanapoibiwa) unaweza kutumia simu hizo kufanya karibia kila kitu Kuanzia kwenye kufanya manunuzi ya vitu,kuelekezwa mitaa, kuangalia barua pepe na hata kuwasiliana na ndugu pamoja na jamaa. Mambo ya kufanya na simu janja ni mengi sana hata nikitaja sitayamaliza. Ukiachana na kila kitu ambacho simu janja yako au tablet inachoweza kufanya inabidi uhakikishe kuna App za muhimu katika simu yako ambazo zitarahisisha ufanyikaji wa mambo hayo kwa namna ya kipekee. KUTAFUTA SIMU ILIYO POTEA/IBWA Hivi unajua hakuna mda mzuri wa kuibiwa? Chochote kama kweli ni chako kikiibiwa lazima uumie sana. Nshashuhudia dada kaibiwa simu akaanza kulia! (hizi smatifoni bwana, Hah!). hapo awali ilikua kama mtu ukiibiwa au ukipoteza simu yako matumaini ya kuipata tena hakuna kabisa Lakini asante kwa Find My iPhone (ya iOS) na Android Device Manager (ya android) sasa tuna matumaini ya kupata vitu...