Skip to main content

App 5 Muhimu Za Kuwa Nazo Katika Simu Janja yako!



Kwa watu wengi sana simu janja zao ndio kila kitu (ukitaka
kuamini angalia sura zao pindi wanapoibiwa) unaweza
kutumia simu hizo kufanya karibia kila kitu
Kuanzia kwenye kufanya manunuzi ya vitu,kuelekezwa mitaa,
kuangalia barua pepe na hata kuwasiliana na ndugu pamoja na
jamaa. Mambo ya kufanya na simu janja ni mengi sana hata
nikitaja sitayamaliza.
Ukiachana na kila kitu ambacho simu janja yako au tablet
inachoweza kufanya inabidi uhakikishe kuna App za muhimu katika
simu yako ambazo zitarahisisha ufanyikaji wa mambo hayo kwa
namna ya kipekee.


KUTAFUTA SIMU ILIYO POTEA/IBWA


Hivi unajua hakuna mda mzuri wa kuibiwa? Chochote kama kweli ni
chako kikiibiwa lazima uumie sana. Nshashuhudia dada kaibiwa
simu akaanza kulia! (hizi smatifoni bwana, Hah!). hapo awali ilikua
kama mtu ukiibiwa au ukipoteza simu yako matumaini ya kuipata
tena hakuna kabisa
Lakini asante kwa Find My iPhone (ya iOS) na Android Device
Manager (ya android) sasa tuna matumaini ya kupata vitu vifaa
vyetu. Kwa kutumia App hizi kuna hati hati kuwa tunaweza kupata
vifaa vyetu kwakufatilia nyendo za simu zetu zilizopotea/ibwa
Find-My-iPhone
Kama App hizo mbili hazitoshi kuna App nyingine inaitwa Prey,
ambayo ni moja kati ya App nzuri za ulinzi na usalama. Prey
inatuma eneo (location) ambalo simu yako iliyoibiwa ipo. Inaweza
pia hata ikapiga picha kwa baadhi ya vifaa kwa kutumia kamera ya
mbele lengo likiwa ni kukutumia picha ya mwizi wako. Pia utaweza
kujua kama mwizi wako anajaribu kubadilisha laini katika simu.
Lakini kama unaona kama haitoshi unaweza ukafuta kila kitu ukiwa
mbali na simu hiyo.
SOMA PIA: Microsoft kuachisha Programu ya Paint katika
Windows 10
PANGILIA PICHA ZAKO
Kama una simu janja hiyo haina ubishi kuwa kuna picha nyingi
sana katika simu hiyo. Kutokana na kuwa na picha nyingi kiasi
hicho kuzipata zile ambazo unataka kutuma kwa familia na marafiki
ni kazi kidogo na hauwezi kufanya jambo hili kwa haraka. Pia
ukiweka picha nyingi sana katika simu yako unaweza ukapata kale
kaujumbe ka “Not Enough Storage Space” kakiwa kanamaanisha
kuwa uhifadhi hautoshi.
Chukua ukurugenzi katika picha zako kwa kutumia App kama Tidy
au Sortpad. App hizi zinakuwezesha kupangilia picha zako katika
ma’Folder’ tofauti au hata kwa makundi vile wewe utakavyo amua.
Vile vile unaweza amua kufuta baadhi ya picha kirahisi
Tidy
Kinachofuata kama kuna picha ambazo usingependa kuzipoteza
milele unaweza ukazihifadhi katika huduma ya hifadhi ya mtandaoni
(cloud service). Google Photos na Room For More yanaweza
yakawa machaguo sahahi kwako.
TAFUTA WiFi
Mara nyingi tuu inatokea , kipindi ambacho unataka WiFi kwa hali
na mali lakini huweza kupata huduma hiyo kwa sababu tuu
umelipita eneo lake linalotakiwa. Hii inaweza ikakutokea wakati
unafanya mambo yako kwa mfao ukiwa unatumia kivinjari kuperuzi
katika mtandao, mara kitu kinakata!. Najua kila mda mtandao
unapokata kisa tuu umepita wigo wa kutumia WiFi unakua
unaudhika kwa kiasi chake.
Kwa kutumia WiFiMapper utakuwa na mkombozi linapokuja swala
zima la kutumia WiFi. Kwa kutumia App hii unaweza kutafuta na
kubaini WiFi ambayo inafaa kutumiwa kati ya zote zilizopo katika
eneo hilo.Unaweza ukagundua WiFi zilizo wazi lakini zenye usalama
mzuri tuu. Ukiwa na App hii utapata huduma ya kimtandao na
hautacheza mbali na App zako muhimu kama vile Facebook,
Instagram na WhatsApp.
WiFiMapper
Pia usipate hofu kwamba huenda unaweza ukajiunga na WiFi
ambayo ina madhara. Kwani WiFiMapper itakuambia kabisa
kwamba mtandao ni wa aina gani.
SOMA PIA: Sasa tumia moja kwa moja GIFs kwenye mtandao
wa Facebook
Pakua WiFiMapper hapa kwa iOS na Android na baada ya hapo
hautakua na haja ya kukosa mtandao wa intaneti katika simu yako.
LINDA MB/GB ZAKO ZA INTANETI
Mpaka ikaitwa simu janja ina maana inaweza fanya kazi nyingi
sana. Lakini lazima tujue kwamba kazi nyingi katika simu janja
zinahitaji uwepo wa mtandao wa intaneti. Fikiria App zako kama vile
WhatsApp, Facebook na App zingine nyingi bila intaneti sio kitu
tena.
Fikiria kutazama video katika Youtube, kwa kifupi yote haya
yanahitaji utumie inteneti yako. Kama una MB/GB za mawazo
inaweza ikawa ni shida kwako kwani utapata tabu katika kupangilia
kipi utumie na kipi usitumie. Mda mwingine MB/GB zako zitaisha
kabla ya muda ambao uliutegemea.
Kuna namna nyingi tuu na tofauti tofauti ambazo unaweza
ukaishiwa MB/GZ zako lakini kwa kutumia App ya Onavo Extend
inaweza ikakusaidia katika hili. App hii kazi yake ni kufinya ‘Data’
ambapo itakuwezesha kupata hadi mara tano ya utumiaji wa MB/
GB zako (haimaanishi kama ukitumia App hii kama ulikua na GB 1
utapata GB 5). Kama simu yako ina uweza wa WiFi basi app hii
itakuunganisha automatiki ili kuhakikisha una sevu MB/GB zako.
Onavo
Pia App hii inaonyesha picha ambazo unataka kuziona tuu, kwa
mfano ukiwa mtandaoni haitafungua picha za chini kabisa ambazo
hujazifikia. Unaweza ukashangazwa vitu vidogo kama hivi vinasevu
‘Data’ zetu kwa kiasi gani. Pia app hii itakupa ripoti ya mwezi ili
kujua ni App gani zinatafuna MB/GB zako kwa sana.
SOMA PIA: Post Picha Moja Instagram Ikiwa Imegawanyika
Katika Vipande Tisa (9)! #Android #iOs
LINDA BETRI LAKO (UWEZO WA KUKAA NA CHAJI)
Simu janja zetu zinafanya vitu vingi sana na vitu vingi vinachukua
sehemu kubwa ya chaji.Hebu fikiria ni App ngapi katika simu yako
zinafanya kazi hata kama hujazifungua na kuzitumia (background
refresh) zenyewe.Kuna App ambazo pia mara kwa mara zinaangalia
eneo gani ulilopo, hata mwangaza katika simu yako ni baadhi ya
vitu tuu ambavyo vitaweza kumaliza chaji ya kifaa chako.
Ndio maana hata katika simu za iPhone ambazo zina matoleo ya
program endashaji za sasa zaidi zina kitu kinaitwa “Low Power
Mode” kwa lengo la kuongeza uhai wa betri.
Kama unahitaji msaada mzuri tuu katika uhai wa betri lako kwa
simu za iOS na Android basi App ya Battery Doctor ndio jibu.
Battery Doctor
Battery Doctor kazi yake ni kusimamia Betri la simu janja yako. Hii
inamaanisha kuwa betri lako halitakufa(isha chaji) kirahisi pale
unapolihitaji kwa hali na mali (labda chini ya 10%). Kwa kifupi App
hii itaweza kuendesha mfumo mzima wa betri katika simu janja
yako.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

JINSI YA KURUDISHA DOCOMENT ZILIZOFUTIKA KATIKA SIMU

Sio kitu kipya wote tumeshawahi fanya, kwa bahati mbaya tulishawahi kufuta taarifa zetu kama vile picha au hata video. Kama ikitokea hivyo tena usikasirike, ITphidel nakuletea njia. Sawa kama nlivyosema kuwa unaweza ukapata taarifa zako zote ambazo ulifuta kwa bahati mbaya lakini kabla ya kuzipata kuna mambo inabidi uyafanye • Usihifadhi (save) kitu kingine chochote katika simu kifaa chako au izime mpaka ukiwa unampango wa kufufua vitu vyako • Zima WiFi na njia za mawasiliano za 2G/3G ili masashisho (update) yanayofanyikaga automatiki yasifanyike. Kumbuka kama yakifanyika, mafaili mapya yanaweza jiweka juu ya yale ambayo unataka kutafufua Tuifahamu Njia Kama Mafaili Yako Yapo Katika Memori Kadi Ukishaona mafaili yako yamefutika bahati mbaya – au hata kwa makusudi – kitu kinachofuata ni kuunganisha kompyuta yako na simu kwa kutumia USB. Kuna baadhi ya matoleo ya vifaa vya android, ukichomeka USB katika kompyuta haijionyesha katika mfumo ule wa ‘kuonekana kama umechomeka Flash tu

TENGENEZA KIPATO KUPITIA FACEBOOK

Mara nyingi wengi wetu tumezoea kutumia social network mbalimbali kama kujiburudisha bila kujua kwamba kila mtandao wa kijamii una njia ya kukutengenezea kipato kikubwa. leo nimeona nianze kukufundisha njia ya kuingiza pesa kupitia facebook  ILI KUTENGENEZA KIPATO KWA NJIA FACEBOOK UNATAKIWA KUWA NA VITU VIFUANTAVYO 1. Unatakiwa uwe na accont ya bank 2.Uwe na creditcard ya mastercard au visacard  3. unatakiwa  uwe na account ya paypal kwa ajili ya kupokea payment kutoka kwenye mtandao wowote wa kijamii utakaojiunga nao ukiwa na hivyo vitu unaweza kutengeneza pesa nyingi kwa mwezi mmoja CHANZO CHA KIPATO Vipo vyanzo vingi au njia nyingi za kutengeneza kipato ndani ya fb leo nitaelezea njia ambayo ni rahisi sana ambayo mtu yeyote anaweza kuitumia bila kuwa mtaalamu sana  njia hiyo ni ya kulipwa kwa like  kwa hiyo unalipwa kwa kupata like unazozipata kwenye page yako au group ndani ya facebook zipo njia kuu mbili za kufanya trick upate like nying  njia ya kwanza ni