Skip to main content

JINSI YA KURUDISHA DOCOMENT ZILIZOFUTIKA KATIKA SIMU

Sio kitu kipya wote tumeshawahi fanya, kwa bahati mbaya tulishawahi kufuta taarifa zetu kama vile picha au hata video. Kama ikitokea hivyo tena usikasirike, ITphidel nakuletea njia.
Sawa kama nlivyosema kuwa unaweza ukapata taarifa zako zote ambazo ulifuta kwa bahati mbaya lakini kabla ya kuzipata kuna mambo inabidi uyafanye
• Usihifadhi (save) kitu kingine chochote katika simu kifaa chako au izime mpaka ukiwa unampango wa kufufua vitu vyako
• Zima WiFi na njia za mawasiliano za 2G/3G ili masashisho (update) yanayofanyikaga automatiki yasifanyike. Kumbuka kama yakifanyika, mafaili mapya yanaweza jiweka juu ya yale ambayo unataka kutafufua
Tuifahamu Njia
Kama Mafaili Yako Yapo Katika Memori Kadi
Ukishaona mafaili yako yamefutika bahati mbaya – au hata kwa makusudi – kitu kinachofuata ni kuunganisha kompyuta yako na simu kwa kutumia USB. Kuna baadhi ya matoleo ya vifaa vya android, ukichomeka USB katika kompyuta haijionyesha katika mfumo ule wa ‘kuonekana kama umechomeka Flash tuu’ .
Kama simu yako haifanyi hivyo na una uhakika taarifa zako hizo zilikuwa katika sehemu ya memory kadi unaweza ukatumia adapta ya memori kadi hiyo na kuichomeka katika kompyuta ili isome mafaili yaliyomo ndani.
Sasa unaweza ukashusha programu ya Recuva katika kompyuta (Unaweza ukashusha ya bure au ya kulipia)
Bofya hapa Kushusha Recuva
Ukishafungua Recuva kitu cha kwanza ni kuchagua mafaili gani unayotaka kuyafufua katika kifaa chako (picha, video n.k). Unaweza ukachagua sehemu husika ambapo unataka mafaili ya eneo hilo yafufuliwe. Kitu cha muhimu cha kuweka akilini hapa ni kwamba program ya Recuva itaonyesha maeneo ambayo inaweza fufua mafaili yaliyofutika tuu.
Recuva Ikionyesha Mafaili Ambayo Unaweza Ukayafufua (Itakubidi kuweka Alama Ya Vyema Katika Mafaili Unayotaka Kuyafufua
Kingine cha muhimu ni kwamba unashauriwa kama ukimaliza fufua mafaili yako inabidi kwanza uyahifadhi (save) katika eneo lingine na kisha baadae ndio uyahamishie katika kifaa chako pale yalipofutika. Kujaribu kuyarudishia pale pale wakati unayafufua kunaweza kukaleta shida wakati mwingine. Kwa mfano kama ukiwa unafufua mafaili yako katika simu janja huna budi kuyahifadhi katika kompyuta yako na yakimaliza kuufufuka uyapeleke tena katika simu.
Kama Mafaili Yako Hayapo Kwenye Memori Kadi (Yapo Kwenye Simu)
Kama mafaili unayotaka kuyafufua yalikuwa katika simu na sio memori kadi basi unaweza kutumia njia hii. Kama hujarihusu njia chaguo la ‘Developer’ katika simu yako fanya hivyo kwa kwenda kwenye Settings > About Phone > Build Number au kwa simu zingine Settings > About Device > Build Number na kisha bofya katika eneo la namba hiyo (Build Number) mara 7. Ukishamaliza kufanya hivyo nenda katika Settings > Developer Options And USB Debugging. Mpaka hapo utakuwa na uwezo wa kutumia programu kama Recuva katika kufufua mafaili
Recuva Ikiwa Inafanya Kazi Yake
Mpaka hapo nadahani umekuwa mtaalamu juu ya jambo la kufufua vitu eeeeh? (haha!). Fufua vitu vyako vya muhimu pindi tuu vinavyofutika kwa bahati mbaya.
Kwa kutumia njia hii huweza ukawa na wasiwasi kuwa utakuja kupoteza vitu vyako na usivipate tena. Kama


Comments

Popular posts from this blog

App 5 Muhimu Za Kuwa Nazo Katika Simu Janja yako!

Kwa watu wengi sana simu janja zao ndio kila kitu (ukitaka kuamini angalia sura zao pindi wanapoibiwa) unaweza kutumia simu hizo kufanya karibia kila kitu Kuanzia kwenye kufanya manunuzi ya vitu,kuelekezwa mitaa, kuangalia barua pepe na hata kuwasiliana na ndugu pamoja na jamaa. Mambo ya kufanya na simu janja ni mengi sana hata nikitaja sitayamaliza. Ukiachana na kila kitu ambacho simu janja yako au tablet inachoweza kufanya inabidi uhakikishe kuna App za muhimu katika simu yako ambazo zitarahisisha ufanyikaji wa mambo hayo kwa namna ya kipekee. KUTAFUTA SIMU ILIYO POTEA/IBWA Hivi unajua hakuna mda mzuri wa kuibiwa? Chochote kama kweli ni chako kikiibiwa lazima uumie sana. Nshashuhudia dada kaibiwa simu akaanza kulia! (hizi smatifoni bwana, Hah!). hapo awali ilikua kama mtu ukiibiwa au ukipoteza simu yako matumaini ya kuipata tena hakuna kabisa Lakini asante kwa Find My iPhone (ya iOS) na Android Device Manager (ya android) sasa tuna matumaini ya kupata vitu

TENGENEZA KIPATO KUPITIA FACEBOOK

Mara nyingi wengi wetu tumezoea kutumia social network mbalimbali kama kujiburudisha bila kujua kwamba kila mtandao wa kijamii una njia ya kukutengenezea kipato kikubwa. leo nimeona nianze kukufundisha njia ya kuingiza pesa kupitia facebook  ILI KUTENGENEZA KIPATO KWA NJIA FACEBOOK UNATAKIWA KUWA NA VITU VIFUANTAVYO 1. Unatakiwa uwe na accont ya bank 2.Uwe na creditcard ya mastercard au visacard  3. unatakiwa  uwe na account ya paypal kwa ajili ya kupokea payment kutoka kwenye mtandao wowote wa kijamii utakaojiunga nao ukiwa na hivyo vitu unaweza kutengeneza pesa nyingi kwa mwezi mmoja CHANZO CHA KIPATO Vipo vyanzo vingi au njia nyingi za kutengeneza kipato ndani ya fb leo nitaelezea njia ambayo ni rahisi sana ambayo mtu yeyote anaweza kuitumia bila kuwa mtaalamu sana  njia hiyo ni ya kulipwa kwa like  kwa hiyo unalipwa kwa kupata like unazozipata kwenye page yako au group ndani ya facebook zipo njia kuu mbili za kufanya trick upate like nying  njia ya kwanza ni